• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe ya ofisi |
Mpanda District Council
Mpanda District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasissi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Fedha na Biashara
      • Mipango, Takwimu, ufuatiliaji na Uchumi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Elimu Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Afya
      • Ujenzi
    • Kitengo
      • Ufugaji Nyuki
      • Uchaguzi
      • TEHAMA na Mahusiano
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Madini
    • Miradi ya Elimu
    • Usafirishaji
    • Ufugaji Nyuki
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Leseni za Biashara
    • Uvuvi
    • Ufugaji Nyuki
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • UKIMWI
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa
    • Fomu
    • Miongozo
    • Matumizi Bora ya Ardhi
    • Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Kitaifa
    • Video za Shughuli za Halmashauri
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha
    • Gazeti la Mpanda Leo
    • Makala Mbalimbali

Miradi inayoendelea

TAARIFA FUPI YA MRADI WA KUPASUA NA KUSAGA KOKOTO KWA KIONGOZI WA MBIO ZA MWENGE WA UHURU KITAIFA NDUGU AMOUR HAMAD AMOUR

Ndugu Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, mradi  huu wa kupasua na kusaga kokoto unamilikiwa na watu tisa waliojiunga katika kikundi kiitwacho YADAMO GROUP KABUNGU. Mradi huu ulianza mwaka 2012 ambapo utafiti wa eneo hili ulionyesha uwepo wa mawe ya kutosha kuanzisha kiwanda hiki. Mradi umeanza rasmi uzalishaji baada ya kusajiliwa mwaka 2016 kwa Reg. Na. BN 17022AA6FB46GB tarehe 24.10.2016 na unalipiwa kodi na tozo mbalimbali kwa mujibu wa sheria.

Ndugu Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, mradi huu umegharimu jumla ya Tshs. 458,000,000.00 ambazo zimegharimiwa na wamiliki wa mradi. Hata hivyo wadau wa mradi huu wanategemea kukopa kwenye taasisi za kibenki kiasi cha shilingi 600,000,000.00 ili kununua mitambo kwa ajili ya kuongeza ufanisi na uzalishaji katika kiwanda hiki. Mpaka sasa kiwanda kimetoa ajira kwa watu 20 hususan vijana.

Ndugu Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, katika eneo hili la mradi tunategemea kujenga uzio kuzunguka kiwanda hiki na pia kujenga nyumba na ofisi za wafanyakazi ili kurahisisha utendaji na kuongeza ufanisi katika uzalishaji. Matarajio ya mradi huu taasisi za umma, makampuni na wajenzi binafsi kutoka nje na ndani ya halmashauri ya wilaya ya Mpanda kununua kokoto zitakazozalishwa na kiwanda hiki.

Ndugu Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, pamoja na ufanisi kiasi uliopatikana katika kiwanda hiki ambao kimsingi ni utekelezaji wa kauli mbiu ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya  ”Tanzania ya viwanda”  changamoto kubwa inayotukabili sisi kama wadau wa maendeleo katika kiwanda hiki ni kukosekana kwa umeme na kulazimika kutumia jenereta ambayo inaongeza  gharama kubwa katika uzalishaji.

Ndugu Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, kwa heshima na taadhima tunaomba utuwekee jiwe la msingi katika kiwanda hiki ambacho kinatarajiwa kuingizia halmashauri ya wilaya ya Mpanda mapato na kutoa fursa zaidi za ajira hasa kwa vijana wa Wilaya ya Tanganyika.

 

 

 

 

 

 

 

Naomba kuwasilisha,                   

  

Mwenge wa Uhuru Oyeeeeeeeee!!!

 


TAARIFA YA MRADI WA UJENZI WA ZAHANATI KATIKA KIJIJI CHA ITETEMYA KATA YA KAREMA KWA KIONGOZI WA MBIO ZA MWENGE WA UHURU KITAIFA NDUGU AMOUR HAMAD AMOUR

 

Ndugu Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, mradi wa ujenzi wa zahanati katika kijiji cha Itetemya tarafa ya Karema unatekelezwa kwa ufadhili wa Serikali kuu kupitia mpango wa kunusuru kaya masikini TASAF III kwa kushirikianana wananchi pamoja na Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda.

GHARAMA ZA MRADI

Mchango wa serikali kuu ni…………………………….Tshs. 66,000,000.00

Mchango wa jamii ni……………………………………..   Tshs.6,891,800.00

Mchango wa halmashauri…………………………….…  Tshs. 3,500,000.00

JUMLA KUU                                                             76,391,800.00

Ndugu Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, lengo la mradi huu ni kutekeleza miradi katika maeneo yenye upungufu wa vituo vya kutolea huduma za afya na elimu kwa walengwa (kaya masikini) kutokana na tathmini ya uwezo wa vituo vya kutolea huduma za afya na elimu iliyofanyika wa kati wazoezi la uandikishaji wa walengwa.

Ndugu Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa, Manufaa ya mradi huu nikupunguza msongamano wahuduma katika kituo cha afya Karema kwa wananchi wa kijiji cha Karema na vijiji vya jirani nakuwawezesha walengwa kutimiza masharti ya afya kwaurahisi zaidi hivyo kuendelea kupata ruzuku kutoka TASAF III ili kutimiza dhana ya mpango ya kunusuru kaya masikini.

Ndugu Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, kwa heshima na taadhima tunakuomba sasa uweke jiwe la msingi katika mradi huu wa zahanati ya kijiji cha Itetemya ambao ukikamilika unatarajiwa kutoa huduma kwa kaya zipatazo 501 pamoja na vijijiji vya jirani.

Naomba kuwasilisha

Mwenge wa Uhuru Oyeeeeeeee!!!!!!!!!

 

 

 

 

TAARIFA FUPI YA MIKOPO YA VIKUNDI VYA WANAWAKE NA VIJANA KWA KIONGOZI WA MBIO ZA MWENGEWA UHURU KITAIFA NDUGU AMOUR HAMAD AMOUR

 

Ndugu kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa, mikopo ya wanawake na vijana ni miongoni mwa miradi ambayo inatekelezwa katika Halmashauri ya wilaya ya Mpanda ili kuwapunguzia wanawake na vijana ugumu wa maisha na kuongeza ajira.

Ndugu Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, katika kipindi cha Julai 2016 hadi Aprili 2017 Halmashauri imetoa mikopo yenye jumla ya shilingi 86,650,000 kwa vikundi vya Wanawake na Vijana. Mchango wa asilimia 5 kwa vijana na asilimia 5 kwa wanawake kutoka katika mapato ya ndani ya halmashauri.

Hadi tarehe 2/4/2017 jumla ya shilingi 56,750,000 zimekopeshwa kwa vikundi vya vijana na wanawake kama ifuatavyo;

 

  • Vikundi 29 vya wanawake kiasi cha shilingi    33,350,000
  • Vikundi 8 vya vijana jumla ya shilingi             23,400,000.

Ndugu Kiongozi wa mbio za mwenge wa Uhuru kitaifa, kwa heshima na taadhima tunakuomba leo tarehe 3/4/2017 ukabidhi hundi 9 zenye thamani ya Tshs. 12,300,000 kwa vikundi 9, ambapo kati ya vikundi hivyo, vikundi 3 ni vya vijana vinavyopokea jumla ya Tshs. 3,700,000 na vikundi 6 vya wanawake vinapokea jumla ya Tshs 8,600,000. Aidha vikundi 4 vya vijana vinapokea pikipiki 8 zenye thamani ya Tshs 17,600,000. Mikopo ina jumla ya Tshs. 29,900,000 ambayo itawanufaisha wanavikundi na itarejeshwa katika kipindi cha mwaka mmoja kwa riba nafuu ya asilimia 10.

Naomba kuwasilisha,

Mwenge wa Uhuru Oyeeeeeeee!!!!!!!!!!!

 

 


 

 


 

 

 

 


Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI ZA MUDA HALIMASHAURI YA WILAYA YA MPANDA September 27, 2019
  • MWALIKO WA UWEKEZAJI UJENZI WA VIBANDA KATIKA MAENEO YA VITUO VYA MAGARI (BUS STAND) LUHAFWE, KASEKESE, MAJALILA NA IKOLA August 29, 2018
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI HALMASHAURI YA WILAYA YA MPANDA September 23, 2019
  • Tazama zote

Habari mpya

  • Kahawa ya Mwese (Tanganyika) yapata soko Ulaya

    July 13, 2019
  • Kilimo cha migomba-Mwese

    July 13, 2019
  • Mpanda DC yakusanya 75.19% ya mapato

    July 12, 2019
  • TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA TASAF AWAMU YA TATU MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASKINI KWA KIPINDI CHA JULAI 2014 HADI APRILI 2019

    May 23, 2019
  • Tazama zote

video

DC wa Tanganyika asisitiza michezo katika kata ya Bulamata
Video nyingine

Mawasiliano ya Haraka

  • Taarifa kwa Umma
  • Orodha ya Madiwani
  • Gazeti la Mpanda Leo
  • Habari Mpya
  • Mwanzo
  • Matukio
  • Matangazo

Kurasa zinazofanana

  • Tovuti ya Ikuli
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi Tanzania
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya TAMISEMI
  • Tovuti ya Takwimu ya Taifa (NBS)
  • Tovuti kuu ya Serikali

Wasomaji Mbalimbali Dunia

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free visitor counters

Dira ya Ramani

Wasiliana Nasi

    Mpandadc

    Sanduku la barua: 1 Mpanda

    Telephone: 025-2820068

    Simu ya mkononi: 0784428273

    Barua pepe: ded@mpandadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Sitemap
    • Huduma
    • Test

Copyright ©2018 mpanda dc . All rights reserved.