• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe ya ofisi |
Mpanda District Council
Mpanda District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasissi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Fedha na Biashara
      • Mipango, Takwimu, ufuatiliaji na Uchumi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Elimu Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Afya
      • Ujenzi
    • Kitengo
      • Ufugaji Nyuki
      • Uchaguzi
      • TEHAMA na Mahusiano
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Madini
    • Miradi ya Elimu
    • Usafirishaji
    • Ufugaji Nyuki
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Leseni za Biashara
    • Uvuvi
    • Ufugaji Nyuki
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • UKIMWI
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa
    • Fomu
    • Miongozo
    • Matumizi Bora ya Ardhi
    • Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Kitaifa
    • Video za Shughuli za Halmashauri
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha
    • Gazeti la Mpanda Leo
    • Makala Mbalimbali

UKIMWI

MUHTASARI WA KIKAO CHA KAMATI YA UKIMWI KILICHOFANYIKA TAREHE 02/01/2018 KATIKA UKUMBI WA IDARA YA MAJI WA  HALMASHAURI YA WILAYA YA MPANDA

     WAJUMBE WALIOHUDHURIA

  • Mh.Diwani.T.Kisesa           - Kata ya Mwese                        -  Mwenyekiti
  • Bi.J.Rupia                        - Kaimu Mkurugenzi Mtendaji      -   Katibu
  • Mh. Diwani.H.Mapengo     - Kata ya Mpanda ndogo
  • Mh.Mbunge. M.Kakoso      -Jimbo la mpanda vijijini
  • Mh. Diwani.O.Sangu         - Kata ya Isengule
  • Mh. Diwani.J.Kansimba     - Kata ya Mishamo
  • Mh.  Diwani S.Kolongo      - Viti maalum Mishamo
  • Mh.  Diwani.P. Pamasi       - Kata ya Katuma
  • Mh.  Diwani.I.Lusambo     - Kata ya Kapalamsenga

 

WAJUMBE (WAALIKWA)

  • Bw.M.H.Mlile                   - Mwakilishi
  • Bw.M.Apolonari               - Mwakilishi
  • Bw.C.Nsokolo                  - Mwakilishi
  • Bi.J.Mrisho                      - Mwakilishi
  • Bi. A.Fundikira                 - Mwakilishi
  • Bw. E.Thobias                 - Polisi
  • Bi.M.Buhele                    - Mwakilishi
  • Mch.A.Palali                    - Mwakilishi
  • Bi.H.R.Sipata                  - Mwakilishi
  • Bw. J.Kabimbi                 - Mwakilishi
  • Bw.A.Silvesto                  - Mwakilishi
  • P.Ndabila                       -  SHIDEFA

 

       WATAALAM WALIOHUDHURIA                           

  •  Bw.F.Msimbe                   - Afisa utamaduni
  • Bi. H.Kitumba               - Kaimu Mkuu wa idara ya Maendeleo na ustawi wa jamii
  • Dr.S.Mtenjela                    - Mganga Mkuu
  • Bi.M.Bukonu                     - Afisa ustawi wa jamii
  • Bw.K.Shilumba                  - Mkuu wa Idara ya Elimu ya Msingi
  • Bw.J.Mwandawila              - Kaimu mkuu wa kitengo cha manunuzi
  • Bw.S.Medda                     - Mkuu wa idara ya utumishi na utawala
  • Bi.T.Mwaikasu                  - Kaimu afisa mipango
  • Bw.M.Lyambilo                 - Mkuu wa Idara ya Elimu ya Sekondari
  • Bw.K.Bulemo                    - Kaimu mratibu wa UKIMWI

 SEKRETARIETI

  • Bi.J.Kahembe                    - Mwandishi wa vikao
  • Bw.P.Kyema                     - Mwandishi wa vikao

 

 

AGENDA NA. HW/MPN/01/01/2018: KUFUNGUA KIKAO.

Katibu alianza kwa kuwasalimu wajumbe na kuwakaribisha kwenye kikao na kuwatakia wajumbe heri ya mwaka mpya.Alimkaribisha Mwenyekiti afungue kikao. Mwenyekiti aliwasalimu wajumbe kwa kuzingatia itifaki na kuwatakia heri ya mwaka mpya. Aliwata radhi wajumbe kwa kikao kuchelewa kuanza huku akisema kuwa ni kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo.Alifungua kikao saa 5:34 asubuhi. 

AGENDA NA. HW/MPN/02/01/2018: KUTHIBITISHA AGENDA

Agenda saba  (07) zilisomwa kwenye kikao na ziliafikiwa. Agenda hizo zilikuwa   Kama ifuatavyo:-

  •  Kufungua kikao
  • Kuthibitisha agenda
  • Kusoma muhtasari wa kikao cha tarehe 02/10/2017
  • Kusoma yatokanayo na kikao cha tarehe 02/10/2017
  • Taarifa ya utekelezaji kwa robo ya pili, 2017/2018
  • Mengineyo kwa idhini ya mwenyekiti
  • Kufunga kikao

 

AGENDA NA. HW/MPN/03/01/2018: KUSOMA MUHTASARI WA KIKAO CHA TAREHE 02/10/2017. 

Muhtasari wa kikao kilichopita ulisomwa,ukaridhiwa kwa ajili ya kumbukumbu za Halmashauri.

AGENDA NA. HW/MPN/04/01/2018: KUSOMA YATOKANAYO 

Utekelezaji wa maagizo ya kikao cha tarehe 02/10/2017 ulisomwa kama ifuatavyo:-

 

SUALA LA MIRADI YA ILANDAMILUMBA SEKONDARI

Ilikuwa imeagizwa kuwa shule ya Ilandamilumba itembelewe kuona miradi yake iliyopo( mradi wa kuku na mbuzi)

UTEKELEZAJI

Ilielezwa kuwa baada ya kutembelea shule hii, timu ilikuta mapungufu katika usimamizi wa klabu na miradi hii haipo. Kutokana na klabu kutosimamiwa vizuri miradi mingi ilikufa.Hata hivyo mwalimu mkuu ameahidi kuboresha klabu hii kwa kuteua mwalimu mlezi mwingine na kusaidia pale inapohitajika.Kitengo cha UKIMWI na idara ya elimu sekondari wataendelea kufuatilia klabu hii na kuirejesha katika uhai wake.Utekelezaji umeafikiwa

SUALA LA WATUMISHI WANAOISHI NA VVU

Ilikuwa imeagizwa kuwa watumishi wanaoishi na VVU huko katani washawishiwe wajitokeze ili kupata takwimu zao halisi. 

UTEKELEZAJI

Ilielezwa kuwa watumishi wanaoishi na VVU/UKIMWI katani ushawishiwa kupitia vikao vya idara zao au mikutano jumuishi.Hata hivyo, suala la kujitokeza ni utashi na maamuzi ya mtu binafsi pasipo kumlazimisha au namna yoyote ya kutumia nguvu.Halmashauri kupitia kitengo cha UKIMWI kwa kushirikiana na idara na vitengo vingine inaendelea kuwasihi watumishi waishio na VVU/UKIMWI kujitokeza ili kupata takwimu sahihi na msaada pale inapohitajika. Utekelezaji haukuafikiwa. Iliagizwa kuwa utekelezaji wa agizo hili uwasilishwe kikao kijacho.Kadhalika,afisa utumishi ashirikishwe kwenye suala hili.

SUALA LA UPIMAJI UNAOFANYIKA KINYEMELA

Ilikuwa imeagizwa kuwa upimaji wa VVU unaofanyika kinyemela kwenye maduka ya dawa Kasekese ufuatiliwe ili kuthibitisha zoezi hili.

UTEKELEZAJI

Ilielezwa kuwa Idara imeandaa utaratibu wa kushitukiza wakati wowote. Utekelezaji uliafikiwa.

SUALA LA MIRADI YA MASHINE KAREMA

Ilikuwa imeagizwa kuwa mradi wa mashine ya kukoboa na kusaga iliyotolewa kwa WAVIU wa Karema ifuatiliwe kujua mustakabali wake.

UTEKELEZAJI

Ilielezwa kuwa baada ya kutembelea mradi, timu ilijiridhisha kuwa mradi upo kwa kuuona, isipokuwa kinu cha kusaga nafaka ni kibovu kutokana na bati zake kuharibika; pia nyumba ya mashine inahitaji kuimarishwa. Hata hivyo, wajumbe ngazi ya kata na tarafa wameomba mradi huu uamishiwe ngazi ya Kata kutoka tarafa ili kurahisisha usimamizi mzuri kutokana na baadhi ya wajumbe kutoka kata za mbali hivyo kushindwa kusimamia mradi vizuri na baadhi ya WAVIU wamekwisha kufariki dunia hivyo kuwa na uongozi mpya. Maelezo ya ufafanuzi zaidi yamo katika taarifa hii na muhtasari wa kuomba kuhamishwa mashine umekwisha wasilishwa. Utekelezaji uliafikiwa.

AJENDA NA. HW/MPN/05/01/2018: TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAPAMBANO DHIDI YA  UKIMWI OKTOBA – DESEMBA ,2017

Taarifa iliwasilishwa kwenye kikao ambayo ilieleza shughuli zilizotekelezwa katika kipindi cha Oktoba - Desemba, 2017 ikiwa ni pamoja na upimaji wa VVU kwa hiari,huduma ya kuzuia maambukizi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto, Taarifa ya Mradi wa mashine ya kusaga na kukoboa nafaka ya watu wanaoishi na virusi vya ukimwi tarafa ya Karema ikiwa na pamoja na changamoto zinazoukabili mradi huo na mapendekezo ya wajumbe, Taarifa ya msaada wa fedha kwa watumishi wanaoishi na virusi vya ukimwi,Utoaji wa vyeti vya uthamini kwa wahitimu wa klabu za ukimwi,ufuatiliaji wa taarifa za klabu kwa shule za sekondari na changamoto zinazozikabili klabu hizo pamoja na utatuzi wa changamoto husika. Kadhalika, taarifa hii ilihusu pia taarifa kutoka kwa waelimisha rika kutoka kata mbalimbali,taarifa kutoka asasi za kiraia,taarifa za utekelezaji kutoka asasi ya KDF, taarifa ya kazi zilizofanywa na dawati la jinsia na watoto katika mapambano dhidi ya VVU na UKIMWI kutoka jeshi la polisi,changamoto mbalimbali zinazokikabili kitengo hiki ziliwasilishwa pia ikiwa ni pamoja na utatuzi wa changamoto hizo. Taarifa ilijadiliwa na kupokelewa na kushauriwa na kuagizwa yafuatayo

 

AGIZO

Takwimu za WAVIU wanaotumia dawa kwa kila kata zipatikane ili kujua hali ya maambukizi katika maeneo yetu hasa kata.

AGIZO

Gharama za kinu cha mashine ya kukoboa Karema ijulikane. Kadhalika,kikao kijacho itolewe taarifa kama mashine hiyo imeanza kufanya kazi au la.

 

AJENDA NA. HW/MPN/06/01/2017:MENGINEYO.

Hakukuwa na mengineyo. Kadhalika,katika kuhitimisha ajenda hii,yafuatayo yalielezwa:

MWENYEKITI WA HALMASHAURI

  • Suala la tisheti na vipeperushi litaingizwa kwenye bajeti ya 2018/2019
  • Vikao vya klabu za ukimwi viwe vinafanyika kwenye shule za sekondari.
  • Kwamba kuna changamoto ya wakunga wa jadi inayochochea maambukizi hivyo ni vyema elimu ikatolewa juu ya suala hili.
  • Ujumbe wa ukimwi ufikishwe kwenye mikusanyiko ya watu kama misibani,disko,harusi ,mikesha. Kadhalika,kondomu zitolewe kwenye mikusanyiko hii.
  • Wajumbe wawe wanafika kliniki na kufikisha elimu ya ukimwi kwa wamama na wababa waliohudhuria kliniki.
  • MHESHIMIWA MBUNGE
  • Aliwatakia wajumbe heri ya mwaka mpya
  • Alimpongeza Mwenyekiti na mganga mkuu kwa kufuatilia na kusimamia miradi ya afya.
  • Ujumbe juu ya maambukizi ya ukimwi upelekwe kwa wananchi kwani hakli ya maambukizi ipo juu.
  • Wazazi waelimishwe juu ya athari za ndoa za utotoni kwa watoto wadogo. Kadhalika,ikigundulika kuwa kuna mtoto kaolewa,taarifa itolewe mapema serikalini ili wahusika washughulikiwe.
  • Mgawanyo wa walimu uangaliwe ili kuhakikisha kila shule ina mwalimu wa kike.

AJENDA NA. HW/MPN/07/01/2018: KUFUNGA KIKAO.

Katibu aliwashukuru wajumbe kwa kuchangia ajenda kwa umakini. Alimkaribisha Mwenyekiti afunge kikao. Kabla ya Mwenyekiti kufunga kikao, Aliishukuru meza kuu kwa mawazo mazuri. Kadhalika, aliwashukuru wajumbe, wawakilishi na wataalam kwa uchangiaji wao mzuri wa ajenda zilizowasilishwa. Alifunga kikao saa 7:30 mchana.

         

Matangazo

  • TANGAZO LA AJIRA YA MKATABA HALMASHAURI YA WILAYA YA MPANDA November 17, 2020
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI December 16, 2020
  • WANAFUNZI WALIYOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA, 2021 HALMASHAURI YA WILAYA YA TANGANYIKA December 19, 2020
  • KUITWA KAZINI WATUMISHI WA KADA YA AFYA HALMASHAURI YA WILAYA YA TANGANYIKA December 21, 2020
  • Tazama zote

Habari mpya

  • Kahawa ya Mwese (Tanganyika) yapata soko Ulaya

    July 13, 2019
  • Kilimo cha migomba-Mwese

    July 13, 2019
  • Mpanda DC yakusanya 75.19% ya mapato

    July 12, 2019
  • TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA TASAF AWAMU YA TATU MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASKINI KWA KIPINDI CHA JULAI 2014 HADI APRILI 2019

    May 23, 2019
  • Tazama zote

video

DC wa Tanganyika asisitiza michezo katika kata ya Bulamata
Video nyingine

Mawasiliano ya Haraka

  • Taarifa kwa Umma
  • Orodha ya Madiwani
  • Gazeti la Mpanda Leo
  • Habari Mpya
  • Mwanzo
  • Matukio
  • Matangazo

Kurasa zinazofanana

  • Tovuti ya Ikuli
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi Tanzania
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya TAMISEMI
  • Tovuti ya Takwimu ya Taifa (NBS)
  • Tovuti kuu ya Serikali

Wasomaji Mbalimbali Dunia

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free visitor counters

Dira ya Ramani

Wasiliana Nasi

    Mpandadc

    Sanduku la barua: 1 Mpanda

    Telephone: 025-2820068

    Simu ya mkononi: 0784428273

    Barua pepe: ded@mpandadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Sitemap
    • Huduma
    • Test

Copyright ©2018 mpanda dc . All rights reserved.