Pichani:Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Mhe.Onesmo Buswelu alipokabidhiwa mkataba wa Utekelezaji wa Afua za Lishe na Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe Mwanamvua Mrindoko 10 Oktoba 2022 katika Ukumbi wa Mpanda Social mara baada ya viongozi hao kusaini Mikataba hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Mhe Onesmo Buswelu amesaini Mkataba wa Utekelezaji Afua za Lishe katika ukumbi wa Mikutano wa Mpanda Manispaa.
Mhe.Buswelu amaesaini Mkataba huo baada ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi kusaini na kuwakabidhi kwa ajili ya kwenda kusimamia utekelezaji wa Afua hizo za Lishe katikaa ngazi ya Wilaya hadi Mtaa.
Akzingumza mara baada ya shghuli za Utiaji sahihi mikataba hiyo ,Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe.Mwanamvua Mrindoko amewataka Wakuu wa Wilaya,Wenyeviti na Wakurugenzi wa Halmashauri kuchukua hatua Kali Kwa Maafisa watakaoshindwa kutekeleza shughuli za uboreshaji Afua za Lishe Mkoani humo.
Mhe. Mrindoko ametoa kauli hiyo katika kikao cha tathimini ya utekelezaji wa mpango mkakati wa usafi na utunzaji mazingira mkoa wa Katavi,kilichofanyika katika ukumbi wa Mancipal Social Hall,Manispaa ya Mpanda.
"Hatutakubali kuendelea kufanyana nae kazi,itabidi apumzike pembeni tutafute Watumishi ambao watasimamia vizuri afua hii ya lishe"
Awali akitoa taarifa ya hali ya Lishe Mkoani humo Afisa Lishe mkoa wa Katavi Asnath Mrema amesema Mkoa wa Katavi uko nafasi ya 14 Kitaifa.
Amesema moja ya sababu ya Mkoa huo kushika nafasi ya 14 ni kutokana na Halmashauri za Mkoa huo kushindwa kutoa fedha za afua za Lishe kama ilivyoainishwa kwenye Bajeti na mipango.
Katika hatua za makusudi,RC Mrindoko amesainiana na kukabidhi mikataba ya Lishe na wakuu wa Wilaya za mkoa huo lengo likiwa ni utekelezaji wa kupambana na lishe duni kuanzia ngazi ya Wilaya hadi ngazi ya kitongoji.
TONGWE - MAJALILA
Sanduku la barua: S.L.P 01 KATAVI - TANGANYIKA
Telephone: +255-252955264
Simu ya mkononi: 0754870344
Barua pepe: ded@tanganyikadc.go.tz
Copyright ©2018 Tanganyika-DC . All rights reserved.