• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe ya ofisi |
Tanganyika District Council
Tanganyika District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tanganyika District Council

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasissi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Fedha na Biashara
      • Mipango, Takwimu, ufuatiliaji na Uchumi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Elimu Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Afya
      • Ujenzi
    • Kitengo
      • Ufugaji Nyuki
      • Uchaguzi
      • TEHAMA na Mahusiano
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Madini
    • Miradi ya Elimu
    • Usafirishaji
    • Ufugaji Nyuki
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Leseni za Biashara
    • Uvuvi
    • Ufugaji Nyuki
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • UKIMWI
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa
    • Fomu
    • Miongozo
    • Matumizi Bora ya Ardhi
    • Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Kitaifa
    • Video za Shughuli za Halmashauri
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha
    • Gazeti la Mpanda Leo
    • Makala Mbalimbali

DC Mhando ahamasisha wananchi kujiunga CHF

Posted on: August 1st, 2017

Kasekese. Mkuu wa wilaya ya Tanganyika Bw. Salehe Mhando amewaagiza wananchi wote waliopo vijiji vyote vya Halmashauri ya wilaya ya Mpanda kujiunga na mfuko wa bima ya Afya ya Jamii (CHF). Mhando ameyasema hayo Julai 29, 2017 wakati wa uzinduzi wa Hamasa ya wananchi kujiunga na bima ya Afya ya Jamii.

Kabla ya kuzindua uhamasishaji, Mhando alizungukia kwanza zahanati ya Kasekese kujionia kama zahanati ina dawa za kutosha na alikuta dawa zipo za kutosha.

“Kabla ya kuanza kuhamasisha wananchi kujiunga na mfuko wa bima ya Afya ya jamii, nimejilizisha kwanza kutembelea zahanati na kuangalia kama zina dawa za kutosha. Nimefika na kukagua zahanati na vituo vya afya vina dawa za kutosha”. Alisema Mhando.

Kila kaya ikichangia shilingi 10,000 kwa ajili ya mfuko wa bima ya afya ya jamii ina uwezo wa kutibisha watu watano kwa mwaka mzima. Katika hali ya kawaida ukichukua elfu 10 ukagawanya kwa watu 5 katika familia utakuta kila mwanachama wa bima anatibiwa kwa gharama ya shilingi 2000 tu.

Katika hao wanachama, mchangiaji anaruhusiwa kuwa na wategemzei wane (4) walio na umri chini ya miaka 18 na wanafunzi wote wa shule za msingi na sekondari wanawawekwa katika kundi la wategemezi. Kwa wale wasio wanafunzi na kama wana umri wa miaka 18 na kuendelea wanapaswa kujiunga na bima ya afya ya Jamii (CHF).

Naye Kaimu Mganga Mkuu wa Halmashauri ya wilaya ya Mpanda Dk.Seleman Mtenjela alishauri wananchi wajiunge kwa wingi kuchangia mfuko wa bima ya afya jamii. Wananchi wakichangia kwa wingi ndivyo na zahanati inavyopata fedha nyingi za kununulia dawa za zahanati au kituo cha afya. Kwa sasa utaratibu umebadilika, kamati za afya zilizopo vijijini ndizo zenye mamlaka ya kuamua matumizi ya ununuzi kwa ajili ya zahanati au kituo.

“Wanachama wakichangia shilingi 5,000,000 na serikali nayo inawachangia 5,000,000. Hii inaitwa tele kwa tele”. Alisema Mtenjela

Hata hivyo, ni vema wananchi wakaelewa kuwa kuna baadhi ya dawa zinazoruhusiwa kuwa kwenye zahanati, zingine kwenye vituo vya afya na dawa zingine zinapatikana kwenye hospitali kubwa tu. Jambo hili linatokana na uwezo wa watalaam wa afya.  Wagonjwa wanapoenda kupata matibabu kwenye zahanati, watalaam wakiwashauri kuwa ugonjwa wao hauna dawa katika zahanati na hivyo hupaswa kuwaelekeza kwenda kituo cha afya au hospitali kwa ajili ya matibabu zaidi.

Serikali ilitangaza watoto watibiwe bure lakini kama wazazi hamtajiunga kwa wingi ili zahanati ipate pesa za kununulia dawa, watatibiwa bure kwa dawa za kutoka wapi? Zahanati ikiwa na dawa za kutosha wale wote wanaostahili kupata matibabu bila malipo wataendelea kuhudumiwa.

Hata hivyo Mkuu wa wilaya ya Tanganyika Bw.Mhando aliwaonya viongozi wa vijiji kuwa makini wakati wa kuhakiki wazee wanaotakiwa kupata matibabu bure.

“Wakati mheshimiwa Rais John Magufuli anashughulika na zoezi la watumishi hewa, kuna wazee hewa katika huduma za matibabu”. Alisema Mhando

Wazee wanaanzia umri wa mika sitini lakini kuna wazee wa miaka 80 ambao ni matajiri. Yaani wana mifugo au uwezo wa kimaisha, sasa watu wa namna hiyo au wenye sifa zinazofanana hatuwezi kuwaruhusu kutibiwa bure.

Wananchi wote wanatakiwa kuwekeza katika bima ya afya ya jamii kwani ugonjwa unajitokeza wakati huna fedha.  Mkombozi wa afya wakati wote kwa mwaka mzima ni mfuko wa bima ya afya ya jamii. Ni muda mwafaka wa kuchangamkia fursa ya kuwekeza katika afya yako na wategemezi 4. Na kama kuna maoni au maswali kuhusiana na mfuko wa bima ya afya ya jamii, fika zahanati au kituo cha afya kilichopo ndani ya wilaya ya Tanganyika kwa ufafanuzi zaidi.

Matangazo

  • WALIOITWA KWENYE USAILI WA NAFASI YA WATENDAJI WA KIJIJI III July 07, 2022
  • WALIOITWA KWENYE USAILI WA NAFASI ZA DEREVA II, KATIBU MAHSUSI III NA WATENDAJI WA KIJIJI III July 07, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA TANGANYIKA July 16, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA TANGANYIKA July 16, 2022
  • Tazama zote

Habari mpya

  • TANGANYIKA KUENDELEA KUWEKA MIKAKATI KUBORESHA SUALA LA LISHE, WAKUU WA IDARA YA ELIMU NA WAKUU WA SHULE WAPEWA MBINU KUSIMAMIA UPATIKANAJI CHAKULA MASHULENI.

    May 13, 2025
  • WABUNGE WA KATAVI, RUKWA NA KIGOMA WATEMBELEA BANDARI YA KAREMA; WAPONGEZA UJENZI WA MELI NA BANDARI YA KISASA.

    May 12, 2025
  • JIMBO LA UCHAGUZI LA MPANDA VIJIJINI LABADILISHWA JINA.

    May 12, 2025
  • KIKAO CHA KUPANDISHA VYEO H/W YA TANGANYIKA CHAFANYIKA

    May 08, 2025
  • Tazama zote

video

MILIONI 328 KUKAMILISHA UJENZI WA OFISI ZA TFS TANGANYIKA, DC BUSWELU ASISITIZA UBORA WA MAJENGO.
Video nyingine

Mawasiliano ya Haraka

  • Taarifa kwa Umma
  • Orodha ya Madiwani
  • WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA HALMASHAURI YA TANGANYIKA
  • Gazeti la Mpanda Leo
  • Habari Mpya
  • Mwanzo
  • Matukio
  • Matangazo

Kurasa zinazofanana

  • Tovuti ya Ikuli
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi Tanzania
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya TAMISEMI
  • Tovuti ya Takwimu ya Taifa (NBS)
  • Tovuti kuu ya Serikali

Wasomaji Mbalimbali Dunia

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free visitor counters

Dira ya Ramani

Wasiliana Nasi

    TONGWE - MAJALILA

    Sanduku la barua: S.L.P 01 KATAVI - TANGANYIKA

    Telephone: +255-252955264

    Simu ya mkononi: 0754870344

    Barua pepe: ded@tanganyikadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Sitemap
    • Huduma
    • Test

Copyright ©2018 Tanganyika-DC . All rights reserved.