Jangiri lakamatwa wilayani Tanganyika na mzigo wa 100 milioni.
Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa wilaya ya Tanganyika, ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Tanganyika Bw. Salehe Mhando ameagiza Aloka Mashaka Kasunzu akamatwe na jeshi la polisi. Aloka Kasunzu amekamatwa julai 30, 2018 baada ya kukutwa na mazao ya misitu yenye thamani ya 100 milioni yaliyovunwa bila kufuata taratibu za uvunaji.
Maamzi hayo yamefanyika Julai 30, 2018 katika kikao cha kamati ya ulinzi na usalama katika ofisi za mkuu wa wilaya –Ifukutwa. Mkuu wa wilaya ya Tanganyika , Bw. Mhando aliwaita watuhumiwa wanne (Aloca M. Kasunzu, Yusuph Ally, Awadh Joackim na Emmanuel Bupe) waliokutwa na mazao ya misitu ambayo hayakufuata utaratibu wa uvunaji.
“Huyu Aloca Mashaka Kasunzu ana ukwasi mwingi lakini unaotokana na mazao ya misitu ya wilaya ya Tanganyika. Sisi tunahangaika wapi pa kupata 500 milioni za kufungua barabara za Mishamo, kumbe kuna majangiri wanaendelea kujinufaisha na mali za Tanganyika. Kuanzia leo, nazuia utoaji wa vibali vya uvunaji hadi hapo tutakapojilizisha kuwa na wavunaji waaminifu. Bora tuwezeshe vijana wetu wa Tanganyika wajiunge katika vikundi ili wachane mbao na kutengeneza samani za shule na zahanati”. Alisema Bw. Mhando
Mazao hayo ya misitu yamekamatwa katika msitu wa Tongwe Mashariki. Tathmini ya awali imeonesha kuwa Aloca Kasunzu amevuna slipa 1936 sawa na shilingi 90,000,000 magogo ya mkurungu 108 sawa na shilingi 10,000,000.
Naye mwenyekiti wa chama cha Mapindunzi katika wilaya ya Tanganyika, mhe. Yasin Kibiriti amesikitika kuona kiongozi wa wananchi anajihusisha na biashara haramu.
Aloca Mashaka Kasunzu ni nani?
Aloca Mashaka Kasunzu ni diwani wa Halmashauri ya wilaya ya Uvinza. Ni mfanyabiashara za mazao ya misitu na biashara za nyumba ya kulala wageni. Ni jangiri wa muda mrefu wa mazao ya misitu yanayopatikana katika Halmashauri ya wilaya ya Mpanda (Tanganyika), hasa katika misitu ya Tongwe Mashariki. Ni mtu asiyefuata wala kutii maelekezo ya viongozi hasa taratibu za uvunaji. Alikatazwa kuvuna miti aina ya Mkurungu, lakini yeye alivuna.
TONGWE - MAJALILA
Sanduku la barua: S.L.P 01 KATAVI - TANGANYIKA
Telephone: +255-252955264
Simu ya mkononi: 0754870344
Barua pepe: ded@tanganyikadc.go.tz
Copyright ©2018 Tanganyika-DC . All rights reserved.