Halmashauri ya wilaya ya Mpanda ina maeneo yanayofaa kwa uwekezaji wa kilimo cha migomba, miti, kahawa na maharagwe. Maeneo hayo yanapatikana katika kata ya Mwese.
Hata hivyo Mwese ina vivutio vingi vya utalii kama vile maji ya mto mapacha ambayo ukiyanywa unapata watoto mapacha, uwanja wa ndege na maajabu yanayopatikana katika mlima Sitwe.