KMCL KUWAINUA WACHIMBAJI WADOGO KATAVI
Mgodi wa Katavi (KMCL) kuwainua kiuchumi zaidi wachimbaji wadogowadogo wote wa mkoani katavi kwa kununua mabaki ya madini. Wachimbaji wadogo ambao wamekuwa wananufaika na kiasi kidogo sana cha madini kutokana na kutumia dhana za kizamani katika shughuli zao za mchakato wa kupata madini. Wamekuwa wanapata kati ya asilimia 25 hadi 30 ya madini baada ya kuchenjua na kutupa mabaki yenye madini kati ya asilimia 70 hdi 75.
Kwa kuwa kampuni ya Katavi mining Co. Limited inatumia mitambo ya kisasa yenyeuwezo wa kuchenjua yale mabaki yote wanayotupa wachimbaji wadogowadogo na kuweza kuyaongezea thamani na kuuzika nje ya nchi, wameona ni bora waruhusiwe kuyanunua kutoka kwa wachimbaji wadogo.
Kikwazo kikubwa cha KMCL ni sheria ya madini na miongozo yake ambayo inawabana. Baada ya KMCL kuwasilisha changamoto hiyo, waziri wa Nchi Ofisi ya Rais uwekezaji, Mhe. Prof. Kitila Mkumbo amemwagiza Mkuu wa mkoa wa Katavi kuhakikisha analisimamia hilo kwa kushirikiana na watu wa madini mkoani Katavi. Tayari ofisi ya madini ipo tayari kutoa ushirikiano na KMCL wameshauriwa kuandika barua ya kuonesha nia ya kufanya biashara hiyo ya mabaki ya madini.
Aidha, baada ya mchakato kukaa sawa ni kwamba wachimbaji wa madini katika maeneo ya Katuma, Mwese, Kapalamsenga na Mnyagala watanufaika na kukuza uchumi wa wahusika. Halmashauri ya wilaya ya Tanganyika imekuwa ikinufaika na kiasi kidogo sana cha makusanyo ya mapato ya ndani yanayotokana na uchimbaji wa madini. Endapo utaratibu wa kuongezeka kwa ununuzi wa mabakia ya madini hayo utaenda kama ulivyopangwa ni matumaini makubwa kwa wananchi kunufaika zaidi.
Hata hivyo muwekezaji wa mgodi wa KMCL ameonesha nia ya kuja na wawekezaji wengi wa kuchimba madini kuja mkoani Katavi. Tanganyika inayo maeneo mengi ambayo kuna madini na wanahitajika wawekezaji zaidi wenye uwezo wa kuchimba kwa njia za kisasa zaidi.
TONGWE - MAJALILA
Sanduku la barua: S.L.P 01 KATAVI - TANGANYIKA
Telephone: +255-252955264
Simu ya mkononi: 0754870344
Barua pepe: ded@tanganyikadc.go.tz
Copyright ©2018 Tanganyika-DC . All rights reserved.