Mkuu wa mkoa wa Katavi Comrade Juma Zuberi Homera amempongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Mpanda Bw. Romuli Rojas John kwa kukusanya shilingi 2,387,392,044.49 sawa na asilimia 75.19 ya mapato ya mwaka wa fedha 2018/2019.
Pongezi hizo amezitoa mwanzoni mwa Julai 2019 alipokuwa anaongea na waheshimiwa madiwani pamoja na watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Mpanda katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Mpanda.
Homera amebainisha kuwa sababu iliyopelekea Halmashauri ya wilaya ya Mpanda kushindwa kukusanya asilimia 100 ni kutokana na serikali kupitia wizara ya maliasili na utalii kuzuia uvunaji wa mazao ya misitu wakati Halmashauri ya wilaya ya Mpanda ilikuwa inatarajia kukusanya zaidi ya shilingi 1,000,000,000 kutokana mazao ya misitu.
Aidha, kuzuiliwa kupigwa mnada kwa mazao ya misitu iliyokamatwa katika msitu wa Tongwe Mashariki kuliathili mapato ya Halmashauri ya wilaya ya Mpanda na kupelekea kushindwa kutekeleza baadhi ya miradi ya maendeleo. Mbao na magogo yaliyokamatwa yana thamani ya zaidi ya milioni 300 na halmashauri imetumia fedha nyingi kuyalinda.
TONGWE - MAJALILA
Sanduku la barua: S.L.P 01 KATAVI - TANGANYIKA
Telephone: +255-252955264
Simu ya mkononi: 0754870344
Barua pepe: ded@tanganyikadc.go.tz
Copyright ©2018 Tanganyika-DC . All rights reserved.