Pichani:Mwenyekiti wa Tume ya Mawaziri Nane ya Utatuzi wa Migogoro ya ardhi na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe.Mwashimba Ndaki akizungumza na Wananchi wa Kata ya Kasekese katika ziara yake kutatua migogoro ya Ardhi Mkoani Katavi.
Serikali imeridhia kufanya upya uhakiki wa ugawaji wa maeneo ambayo yameonekana kuwa na migogoro ya ardhi mkoani Katavi.
Akizungumza baada ya kutembelea baadhi ya maeneo hayo ikiwemo eneo la Visima Viwili lililopo katika Kata ya Kasekese wilayani Tanganyika,Mwenyeketi wa kamati ya mawaziri nane wa kisekta ambaye ni Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki ameelekeza kufanyika upya tathmini kwa maeneo yote Mkoani Katavi yenye migogoro ya mipaka baina ya Wananchi na Mamlaka za Uhifadhi ili kuja na suluhu ya kudumu ya kuondoa Migogoro hiyo
Aidha Mhe.Ndaki amewaomba Wananchi Wilayani Tanganyika Mkoani Katavi kuepuka kuendelea kufanya shughuli za makazi katika maeneo ambayo hawana uhakika wa kuendelea kuishi kusudi kuepuka usumbufu na wakati mwingine hasara zisizokuwa na ulazima.
Awali akizungumza wakati wa utambulisho Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe.Mwanamvua Mrindoko aliiomba tume hiyo ya Mawaziri Nane inayozunguka Nchi nzima kutatua Migogoro mbalimbali ya ardhi kuharakisha utatuzi wa migogoro mbalimbali ya ardhi inayoendelea baina ya Wananchi na maeneo ya hifadhi Mkoani Katavi ili kutoa fursa kwa Wananchi kufanya maandalizi ya mashamba kwa wakati ili kuendana na msimu wa Mvua ambao umekaribia.
Kwa upande wao wananchi wameomba kamati hiyo kushughulikia kwa haraka jambo hilo ambalo limekuwa likisababisha migogoro inayojirudiarudia.
Kamati hiyo ya Wizara nane za kisekta imeundwa na Wizara ya Maliasili na Utalii, Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Wizara ya Kilimo na Ushirika, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Ofisi ya Rais TAMISEMI na Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira)kwa ajili ya kutembelea maeneo yenye migogoro ya ardhi nchini na baadae kutoa mapendekezo ya namna ya kusuluhisha migogoro hiyo.
TONGWE - MAJALILA
Sanduku la barua: S.L.P 01 KATAVI - TANGANYIKA
Telephone: +255-252955264
Simu ya mkononi: 0754870344
Barua pepe: ded@tanganyikadc.go.tz
Copyright ©2018 Tanganyika-DC . All rights reserved.