Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Bw.Onesmo Buswelu amewataka Wananchi Wilayani humo kutoa ushirikiano kwa Wataalamu wa Afya ili kufanikisha zoezi la Utoaji wa Chanjo ya matone ya Ugonjwa wa POLIO litakaloanza mapema 1 Septemba 2022.
Bw.Buswelu ametoa rai hiyo wakati akipokea taarifa ya Maandalizi ya zoezi hilo katika ukumbi wa Mikutano wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika,kikao kilichokutanisha Wakuu wa Idara na vitengo,pamoja na Waratibu wa zoezi hilo ngazi ya Halmashauri.
Mratibu wa huduma za chanjo Tanganyika Bw.Philip Mihayo ameeleza kikaoni hapo kuwa Halmashauri ya Wilaya Tanganyika ina lengo la kuwachanja watoto 73,251 kwa marudio wenye umri wa miezi 0 mpaka 59 (Chini ya miaka 5)
Ameeleza kuwa Watoto hao watafikiwa nyumba kwa nyumba Ikihusisha pia utoaji wa chanjo katika vituo vya muda katika maeneo mbalimbali (masoko, shule, misikiti, makanisa, mashambani, vituo vya mabasi, makambi ya wakimbizi, makambi ya wavuvi na wakataa mikaa); vituo vya mipakani (transit sites).
Halmashauri ya Wilaya Tanganyika imepokea fedha toka UNICEF kiasi cha Tsh. 39,175,250 kugharimia mafunzo na uhamasishaji katika jamii na pia WHO itatoa kiasi cha Tsh. 74,562,100 kugharimia usafiri, mafunzo na uchanjaji kwa kuwalipa wahusika moja kwa moja kupitia namba zao za simu.
Raslimali watu: Jumla ya watu 548 ambao ni Watoa huduma za Afya 166, wachukua taarifa 166, wahamasishaji 166, viongozi wasimamizi 44 na wasimamizi huru 6 watashiriki moja kwa moja katika kufanikisha kampeni hii
TONGWE - MAJALILA
Sanduku la barua: S.L.P 01 KATAVI - TANGANYIKA
Telephone: +255-252955264
Simu ya mkononi: 0754870344
Barua pepe: ded@tanganyikadc.go.tz
Copyright ©2018 Tanganyika-DC . All rights reserved.